Aliyekuwa mke wa Donald Trump afariki dunia

Aliyekuwa mke wa Donald Trump afariki dunia

Moja kati ya taarifa kubwa ya kimataifa ni hii hapa inayomuhusu Ivana Trump ambaye amewahi kuwa mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, amefariki dunia Julai 14, 2022 nyumbani kwake New York City, nchini Marekani.


Ivana aliyefariki akiwa na umri wa miaka 73, alikuwa ni mke wa kwanza wa Donald Trump ambapo walifunga ndoa yao mnamo mwaka 1977 na kufanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Donald Jr, Ivanka na Eric kabla ya ndoa kuvunjika na kupelekea kuachana kwao mnamo mwaka 1992.



Taarifa hiyo imetolewa na Donald Trump kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii unaojulikana kama Truth Social ambao ni mali ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, taarifa hiyo ilisomeka kama ifuatavyo “Ninayo huzuni kubwa kuwafahamisha wote mliompenda, ambao ni wengi kwamba Ivana Trump amefariki dunia nyumbani kwake jijini New York, alikuwa ni mwanamke mzuri na wa ajabu, ambaye aliishi maisha mazuri na yenye hamasa kubwa, fahari na furaha yake kubwa walikuwa ni watoto wake watatu, Donald Jr., Ivanka, na Eric, alijivunia sana wao , kwani sote tulijivunia yeye. Pumzika kwa Amani, Ivana.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags