Akili Bandia Sasa Inaweza Kukutunzia Taarifa Binafsi

Akili Bandia Sasa Inaweza Kukutunzia Taarifa Binafsi

Watumiaji wa Akili Bandia (AI) katika mitandao yao ya kijamii kama vile WhatsApp, Instagram na Facebook Messenger wataweza kutunza taarifa zao binafsi ambazo wataziweka katika mitandao hiyo.

Taarifa hizo ni kama vile dini, sehemu unapoishi, vitu unavyopendelea kuvifanya na kula, siri zako binafsi pamoja na taarifa nyingine ambapo baadaye utakapo zisahau utauliza Akili Bandia na itakupatia majibu.

Njia ya kuilisha taarifa zako itafanyika kwa njia ya mazungumzo ya moja kwa moja. Hata hivyo Akili Bandia hiyo inayojulikana kama ‘Chatbot’ inauwezo wa kutambua aina yako ya uulizaji maswali.

Mtu mwingine akitumia haitompatia majibu sawa. Aidha utakuwa na uwezo wa kuilisha taarifa zako na kisha kuzifuta.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags