Ishu Ya Wema Kuachana Na Whozu Ipo Hivi

Ishu Ya Wema Kuachana Na Whozu Ipo Hivi

Moja ya stori inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na staa wa Bongo Movie Wema Sepetu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Whozu.

Kutokana na wadau na mashabiki mbalimbali kuuliza sababu ya wawili hao kuachana Mwanaspoti ilipata muda wa kuzungumza na mwigizaji huyo huku akiweka wazi kuwa hawezi kuzungumza habari hizo na kama zipo basi yeye atakuwa hana bahati ya kukaa na mwanamume.

“Hapo unadhani mimi naweza kuongea nini? Mimi nina mambo mengi ya kufanya bwana, haya mambo ya mapenzi na maswali yako yaache kwanza, hizo habari ziko mitandaoni, ziache ziishie huko huko mtandaoni na acha ziwe hivyo na kwenye mapenzi hayo mambo yapo, yanawatokea watu wengi.

Ila mimi kama ikiwa hivyo basi nitakuwa sina bahati ya kukaa na mwanamume, kila nikikaa naye baadaye tunakuja kutofautiana, hicho ndicho kitu kikubwa kwa sababu pesa najua kutafuta, kama maisha ninayoishi najimudu, kwanza kwa nini kila mara nimekuwa nikilizwa na mapenzi jambo ambalo husababisha najiona sina bahati kwa kusalitiwa ama kunyanyaswa na wanaume," alisema Wema.

Tetesi za kuachana kwa wawili hawa ni nyingi, ila Sababu kubwa iliyotajwa ni usaliti unaofanywa na Whozu jambo ambalo lilipelekea Wema kumtimua Whozu nyumbani kwake. Wawili hao walianzisha uhusiano wao na kuweka wazi katika mitandao ya kijamii mwaka 2022.

Mbali na hayo lakini pia Mama mzazi wa Wema hakuwa amebariki mahusiano hayo akidai Whozu kuishi nyumbani kwa binti yake bila kutambulishana kwa wazazi ni kosa na anatakiwa afuate taratibu za kujitambulisha ukweni, huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa huwenda suala hilo likawa ndio chanzo cha kutemana kwao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags