Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameeleza kwa mara ya kwanza, nini kilisababisha aondoke bila kutumbuiza kwenye usiku wa tuzo za Trace zilizotolewa Zanzibar Februari 26, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 15, 2025, King Kiba amesema sababu ya kukwepa kutumbuiza ni baada ya kuona baadhi ya watu wapo kama mtego katika shoo hiyo.
“Nadhani ile ishu haikuwa organised na Trace kwa sababu kuna watu tu walikuwepo unaona kama ni mtego kabisa, kila aliyekuwepo pale wanajua. Nikajua kabisa hapa kuna mtego,” amesema King Kiba.
Amesema alikuwa akifanya mawasiliano na wasimamizi wa shoo hiyo lakini baadaye alipokea taarifa ambazo zilikuwa na mkanganyiko.
“Nilitakiwa niimbe live nikaambiwa nipeleke wimbo wangu kwa The Composers ili waweze kujua watautumiaje. Ila nilivyofika kwenye hoteli nikaambiwa ratiba yangu ya mazoezi itakuwa siku inayofuata baada ya hapo nikaenda kula. Nimemaliza nikaambiwa ratiba yangu itakuwa ni baada ya masaa matatu mbele nikaona sawa haina shida nikaenda. Tukaanza kujiandaa nimefika pale nikapigiwa simu na mtu kuwa bwana hatufanyi live tena,” amesema Alikiba.
Utakumbuka, Alikiba alikuwa kati ya wasanii waliotakiwa kutumbuiza kwenye tuzo za Trace Music Award zilizofanyika Februari 26, 2025. Lakini aliondoka bila kupafomu, kitu ambacho kiliacha maswali mengi kwa wahudhuriaji na mashabiki wa muziki.

Leave a Reply