Peter Asimama Mahakamani Kutoa Ushahidi Dhidi Ya Kaka Yake

Peter Asimama Mahakamani Kutoa Ushahidi Dhidi Ya Kaka Yake

Mwanamuziki Peter Okoye ‘Mr P’ ambaye alikuwa mmoja wa wasanii katika kundi la P-Square, ameibua taharuki baada ya kuwa shahidi katika kesi ya kaka yake Jude Okoye, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutakatisha fedha.

Kesi hiyo, ambayo ilianza kusikilizwa jana Jumatatu Aprili 14,2025 katika Mahakama Kuu ya Shirikisho jijini Lagos, imeibua mijadala baada ya Peter kutoa ushahidi kwa kaka yake akikiri kutumia fedha za kundi bila kuwataarifu.

Mr P alieleza kuwa Jude ambaye alikuwa msimamizi wa fedha za P-Square, alianzisha kampuni iitwayo Northside Music Limited ili kukusanya malipo ya mirabaha (royalties) bila ya yeye na Poul kujua lolote

Aidha aliendelea kwa kudai matendo ya Jude yalimuweka gizani kuhusu fedha za kundi hilo, na alilazimika kuchukua hatua kali ili kugundua ukweli. Huku akiweka wazi hata alipomuomba fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake Jude alikata akisema ‘Ukiondoka P-Square, umeondoka na hela pia’.

Pia alitoa ushahidi kuwa kaka yao Jude kumiliki akaunti zote za Bank ikiwemo Ecobank, Zenith, na FCMB jambo ambalo lilisababisha kundi la P-Square kuvunjika kutokana na kutokuwa na fedha za kufanyia maendeleo.


“baada ya kundi kurudi tenda mwaka 2021 tuliendelea na biashara yetu, lakini tukaanza kuwa na matatizo kuhusu jinsi alivyokuwa anaendesha mambo. Kero kubwa ilikuwa yeye kuwa msaini pekee kwenye akaunti zetu zote za benki zikiwemo Ecobank, Zenith, na FCMB. Akaunti zote zilimilikiwa na kampuni yake,”amesema Peter

Zaidi ya hayo, alimuhusisha mke wa Jude katika jesi hiyo akifichuwa kuwa anamiliki asilimia 80 ya ‘Northside Music Limited’, huku Jude akiwa na asilimia 20. Peter alidai alipowasilisha ombi la kupata taarifa za mapato, zilikuwa zikichezewa, hali iliyopelekea kupungua kwa mapato na kupoteza fursa mbalimbali za kibiashara.

Kutokana na shtaka hilo Tume ya Kupambana na Ufisadi (EFCC) inamshutumu yeye na kampuni yake kwa makosa ya kutakatisha fedha zaidi ya dola milioni 1 za Kimarekani.

Hata hivyo, Jude Okoye amekana mashtaka yote na amejibu “siyo kweli” kwa kila shtaka, huku kesi hiyo ikipelekwa mbele hadi Juni 4 kwa ajili ya hoja za upande wa utetezi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags