Baddest 47 Azidi Kuipa Nguvu Singeli

Baddest 47 Azidi Kuipa Nguvu Singeli

Wakati muziki wa Singeli ukiwa mbioni kutangazwa rasmi kuwa sehemu ya Orodha ya Urithi wa Dunia, kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi, wasanii wa Dancehall na Bongo Fleva nao wana mchango mkubwa katika ukuaji wa muziki huo.

Ukiachana na D Voice ambaye amekuwa akichanganya Bongo Fleva na Singeli, pia yupo mkali wa Dancehall nchini, Baddest 47, ambaye naye amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa Singeli na kuusukuma kufika kimataifa.

Kama utani safari yake ya kujiingiza katika muziki wa Singeli ilianza miaka mitatu iliyopita akipewa shavu na D Voice kupitia singeli iitwayo ‘Mchanganyiko’ ambao D Voice aliutoa kabla ya kusainiwa na lebo ya WCB.

Aliendelea na mchakato huo huku akishirikishwa tena kwenye Singeli ya ‘Tai Chi’ na mwanamuziki Balaa Mc. Ngoma ambayo iliachbiwa miaka miwili iliyopita na mpaka kufikia sasa ikiwa imetazamwa mara milioni 1.4 katika mtandao wa YouTube.

Lakini pia hakuishia hapo miezi sita iliyopita alitia mistari yake katika Singeli ambayo iliuwa sana katika mitandao ya kijamii ya ‘Wivu’ iliyotazamwa mara milioni 5.2 YouTube akishirikiana na mastaa kama Dj Mushizo, Ibraah pamoja na Jay Combat.

Aidha aliendelea kuingiza mistari katika muziki wa Singeli uweze kutambulika zaidi sauti yake ikisika tena katika ngoma ya ‘Sio Mwana’ akishirikishwa na Dakota pamoja na Gnako. Vile vile akisikika tena kwenye singeli ya ‘Mapenzi Hisia’ iliyoachiwa mwezi mmoja uliyopita ikiwakutanisha wasanii kama Dj Mushizo, Jetty Mc, Vanillah na Jay Combat.

Utakumbuka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi, Mei 7,2025 akiwa Bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 alieleza kuwa muziki wa singeli upo mbioni kutangazwa duniani.

"Wizara kwa kushirikiana na UNESCO, iliratibu warsha ya wadau ya uteuzi wa muziki wa singeli kuorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia unaoratibiwa na UNESCO. Warsha hiyo ilifanyika Machi 24-25, 2025 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 120 kutoka Wizara, taasisi na wadau wa sekta ya utamaduni wa mikoa mbalimbali nchini.

"Muziki wa Singeli, unatumia vionjo vya ngoma za asili ikiwamo midundo na mikong’oso. Midundo ya Singeli imeendelea kuzalishwa kwa wingi kupitia kivunge cha mtozi kilichotengenezwa na BASATA.

"Upekee wa Singeli umeifanya kuwa kivutio kikubwa katika matamasha makubwa ya kimataifa kama vile “Nyege Nyege” Festival nchini Uganda, DUO Festival nchini Ubelgiji, Primavera Sound Festival Nchini Hispania, Apporlibation Festival nchini Ujerumani na Cora Festival nchini Ufaransa,"amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags