Kim Kwenda Na North Met Gala, Kanye Awaka

Kim Kwenda Na North Met Gala, Kanye Awaka

Mwanamuziki kutoka Marekani, Kanye West ameonesha kutofurahishwa na malezi ya aliyekuwa mke wake Kim Kardashian kwa watoto, hii ni baada ya Kim kwenda na North West kwenye maonyesho ya Met Gala.

Kwa mujibu wa TMZ, Kanye aliwasilisha barua mahakamani kupitia wakili wake, Kathy Johnson, akimtaka Kim kuheshimu makubaliano waliyoweka wakati wa talaka, huku akimtaka pia aache kuwatumia watoto wao kwa manufaa binafsi.

“Mei 5, 2025, mteja wako alimsafirisha North West hadi Met Gala huko New York City, na kumweka wazi kwa umakini mkubwa wa vyombo vya habari.

“Ripoti zinaonyesha kuwa North aliachwa bila uangalizi ndani ya gari wakati wa tukio hilo, jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kama hatari kwa mtoto. Hili ni kinyume na makubaliano ya pamoja ya ulezi, ambayo yanawataka wazazi wote wawili kutoa mazingira salama na yenye uangalizi kwa watoto wao.” Imeeleza taarifa hiyo

Barua hiyo inaendelea: “Uwepo wa North katika tukio la hadhara lenye paparazi na waandishi wa habari wengi, bila idhini ya mzazi wa pili, ni ukiukwaji wa haki za mzazi huyo kwa mujibu wa makubaliano ya talaka. Pia, video na picha za North zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii bila ridhaa ya mteja wangu, jambo ambalo tayari amelipinga hadharani mara kadhaa.

Utakumbuka, Kim na Kanye walitalikiana mwaka 2021 baada ya kudumu kwenye ndoa miaka 7 huku wakifanikiwa kupata watoto wanne. Kama sehemu ya makubaliano ya talaka yao, walikubaliana kuwa na ulezi wa pamoja wa watoto, na Kanye analipa dola 200,000 kila mwezi kama pesa za matunzo ya watoto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags