Hatimaye mwanamuziki Beyonce ameshinda kipengele cha Albamu Bora ya Mwaka ‘Cowboy Carter’ katika tuzo za Grammy 2025 Best na kuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kushinda kipengele hicho.
Beyonce ambaye anashikilia rekodi ya msanii anayeongoza kuwania tuzo hizo kwa mara 99 pia ndiye msanii anayeshikilia rekodi ya msanii aliyechukua tuzo za Grammy mara nyingi zaidi akibeba mara 34 ndani ya miaka tofauti tofauti.
Katika tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Februari 3,2024 katika ukumbi wa Crypto.com huko Los Angeles amenyakua kipengele cha Best Country Albamu na Best Country Group Perfomance
“Ningependa kuwashukuru familia yangu nzuri. Wote wasanii walioshirikiana nami. Asanteni. Albamu hii isingekuwa hivi bila ninyi. Ningependa kumshukuru Mungu tena, na mashabiki wangu. Bado nipo kwenye mshtuko, hivyo asanteni sana kwa heshima hii,” amesema Beyonce wakati akichukua tuzo yake
Utakumbuka licha ya Beyonce kutoa albamu nyingi zilizofanya vizuri duniani, hii ndiyo inakuwa mara ya kwanza kushinda kipengele cha Albumu Bora.
Tayari ametoa albamu nane za studio, albamu tano za moja kwa moja LIVE Album, albamu tatu za mkusanyiko, EP tano, albamu moja ya sauti na albamu mbili za karaoke.
Ameuza zaidi ya rekodi milioni 200 duniani kote, na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wa muziki wanaouza zaidi wakati wote.
Leave a Reply