Albam hiyo ambayo imechiwa siku moja iliyopita imeripotiwa kukimbiza katika majukwaa mbalimbali ya kuuza na kusikiliza muziki ikiwa ni pamoja na Spotify, Apple Music na YouTube, huku mashabiki wakimsifu kwa ubunifu aliouonyesha katika kazi hiyo mpya.
Aidha wakati alipokuwa kwenye mahojiano na Apple Music, Bieber ameeleza dhumuni la kutoa album hiyo akieleza kuwa ni kutoa ujumbe utakaogusa maisha ya kila mtu.

“Nimeweka moyo wangu wote katika albamu hii. Kila wimbo una sehemu ya maisha yangu. Natarajia kila mtu atajiona ndani ya kazi hii,”amesema Beiber
‘SWAG’ imekuwa album tofauti na zile alizowahi kuachia hapo awali kwani amechanganya radha mbalimbali ikiwemo R&B, Hip Hop na Afrobeat huku akiwashirikisha mastaa wakubwa kama Drake, Burna Boy, Doja Cat na SZA.
Kupitia album hiyo kwenye baadhi ya nyimbo zake kama ‘Mirror Talk’ na ‘Unfiltered’, Bieber ameeleza changamoto alizokumbana nazo za afya ya akili, maisha ya ndoa pamoja na safari yake ya kumrudia Mungu.
Hata hivyo wachambuzi wa muziki kutoka Marekani wanaeleza kuwa Bieber atafanikiwa kulifufua jina lake katika muziki kwa mara nyingine kupitia album hiyo ambayo tayari imeingia nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200.
Aidha kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bieber amethibitisha kuwa ataanza ziara ya dunia (SWAG World Tour) mwishoni mwa mwaka huu, akitarajiwa kupiga show katika miji kama London, Tokyo, Lagos, na Rio de Janeiro.
Leave a Reply