Mwanamuziki Chris Brown amewashtaki watayarishaji wa makala inayoeleza unyanyasaji aliyowahi kuufanya, iitwayo ‘Chris Brown: A History of Violence’ akidai kuwa makala hiyo imejaa madai ya uongo.
Kufuatia hati mpya zilizowasilishwa mahakamani Breezy anaishutumu Warner Bros. Discovery, Ample, na wengineo kwa kueneza na kuchapisha madai ya kashfa kwake huku akiweka wazi kuwa makala hiyo haina ukweli wowote ni ya uongo.
Utakumbuka kuwa mfululizo wa makala hiyo ulijikita zaidi kwenye unyanyasaji ambao Breezy aliwahi kumfanyika aliyekuwa mpenzi wake Rihanna tukio lililotokea mwaka 2009.
Hata hivyo katika maelezo aliyoyawasilisha mahakamani Breezy aliweka wazi kuwa tayari amewajibika kwa makosa hayo ya zamani hivyo waandaaji wa makala hiyo hawakutakiwa kurudisha tena mkasa huo hivyo amefungua mashitaka hayo kwa lengo la kudai fidia ya kumchafua kiasi cha dola 500 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 1.2 trilioni.
Rihanna na Breezy walianzisha uhusiano rasmi mwaka 2008 hadi 2012, Brown alikamatwa kwa kumshambulia Riri mwaka 2009 licha ya hayo wawili hao walirudisha tena uhusiano wao huku wakitemana rasmi 2012
Leave a Reply