Diamond Alivyotumia Show Ya Jux Kumaliza Ugomvi Na Zuchu

Diamond Alivyotumia Show Ya Jux Kumaliza Ugomvi Na Zuchu

Mwanamuziki ambaye anatambulika Kimataifa kupitia wimbo wake wa ‘Komasava’, Diamond ameonekana kutumia show ya Jux kumaliza ugomvi wake na Zuchu.

Show hiyo ambayo imefanyika usiku wa kuamkia leo Februari 22, 2025 ‘Coco Beach’ wawli hao wameonekana pamoja kwenye kila hatua jambo ambalo limezua mijadara kupitia mitandao ya kijamii ka kuyananga mahusiano hayo.

“Yaani zuchu haoni aibu, Priscilla, yeye anandoa, but king"ang'a yeye kutumika tu”, “Ila king'ang'anizi ana moyo wa chuma nyie”, “Ila twende nyuma turud mbele zuchu anamdhalilisha mama ake,” huku wengine wakionesha kufurahishwa na penzi hilo kwa kuandika.

“Hawa kuwatenganisha labda mahakama iingilie kati”, “Mange aje na lingine Sasa, waache kuingilia mapenzi ya watu alafu wasikalili maisha kisa Diamond alichezea wengine eti na zuchu atachezewa mambo yanabadilika,”.

Aidha ugomvi wa wawili hao ulianza mwenzi uliyokwisha jambo ambalo lilipelekea Zuchu kufuta utambulisho wake kama yeye ni msanii wa lebo ya WCB ambapo mpaka kufikia sasa bado hajarudisha utambulisho huo.

Baada ya ugomvi wa wiki kadhaa ndani ya mwezi huu walionekana pamoja kwenye matamasha mbalimbali likiwemo Dodoma, Sherehe ya harusi ya Jux na Priscilla na sasa kwenye show ya Jux ambapo imewaonesha wawili hao kuwa sawa licha ya kuzuga gumzo mitandaoni kuhusu Simba na ex wake Ritha.

Mbali na wawili hao kuonekana kumaliza tofauti zao lakini pia kupitia mitandao ya kijamii kunasambaa sauti ya mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa akiweka wazi kuwa yupo tayari kumtolea mwanae kiasi chochote ili ameweze kutoka WCB.

“Kama umeambiwa kwenye Lebo yao hawamtaki pia niambie sasa hivi tupotayari kutoka kwenye hiyo Lebo, wakati wowote kama asubuhi na pesa zozote watakazo zitaka tutalipa,” amesema Khajida Kopa kwenye moja ya video yake inayotrend katika mitandao ya kijamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags