Nyota wa muziki nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' amesema atawasaini kwenye rekodi lebo ya WCB, waliokuwa washiriki wa mashindano ya kusaka vipaji (BSS) Moses Luka (DRC) na Saluh Kulwa.
Diamoond ameyasema hayo Februari 28,2025 akiwa katika fainali ya mashindano hayo ambayo alihudhuria kama mgeni rasmi.
"Mimi leo hapa kuna vijana wawili nimewaona na siyo kuwaona nimetamani kuwasaini mtakapomaliza mchakato wenu nitawaomba mimi nikae nao, tukiridhiana basi tuwasaini Wasafi.
"Natambua changamoto za kuhangaika kwenye muziki kutoka. Kwa hiyo mtu anapopata nafasi kama BSS inakuwa amepata kitu kikubwa sana. Mimi majaji waliokaa pale huwa nawaheshimu sana, huwa najifunza mambo mengi kupitia kwao. Muziki wangu najifunza kupitia maneno yao,"
Amesema miaka ya nyuma wakati anajitafuta kimuziki alishauriwa kushiriki BSS lakini aliogopa.
"Washiriki ambao hawajabahatika nataka watambue wao kushiriki tu BSS ni washindi. Mimi wakati najitafuta kuna mtu niliomba anisaidie nitoke kimuziki akaniambia kama kweli najua nije kwenye mashindano ya BSS.
"Nilikimbia niliogopa hata kusogea hapa sikuweza, nilikuwa naogopa ila wapo wameweza kusogea basi ni washindi,"amesema
Hata hivyo alimalizia kwa kuweka wazi kuwa wasanii hao anaotamani kuwasaini Wasafi ni mshindi wa pili na wa kwanza ambao ni Moses Luka na Saluh Kulwa

Leave a Reply