Diddy Na Cassie Wafunguliwa Mashtaka

Diddy Na Cassie Wafunguliwa Mashtaka

Wakati kesi ya mkali wa muziki wa hip hop, Sean "Diddy" Combs ikikalibia kutamatika huku hukumu ikitarajia kutolewa Octoba mwaka huu, sakata jingine limeibuka ambapo mwanaume mmoja aitwaye Clayton Howard amefungua kesi dhidi ya Diddy na mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura.

Katika kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani na kuripotiwa na TMZ, Howard ambaye alijulikana kwa jina la ‘Dave’ alikuwa akifanyakazi kwa ajili ya matukio ya ngono ya kulipwa kwa niaba ya Diddy.

Howard anadai kuwa aliambukizwa ugonjwa wa zinaa kupitia mahusiano ya kingono na Cassie, na baadaye aligundua kuwa alimpa mimba, lakini hakuwahi kuelezwa kuhusu mimba hiyo hadi alipobaini kuwa Cassie alitoa mimba hiyo bila kumshirikisha.

Kesi hiyo imeibua mshtuko mkubwa huku Howard akitambulika kama mmoja kati ya wanaume saba waliotajwa na waendesha mashtaka wa shirikisho kuwa walihusika katika kusafirishwa kutoka jimbo moja hadi jingine kwa ajili ya matukio ya ukahaba.

Utakumbuka Julai 2,2025 jopo la majaji wakiwemo wanaume nane na wanawake wa nne walitoa uamuzi rasmi ukieleza kuwa msanii huyo amekutwa na hatia katika mashtaka mawili kati ya matano yaliyokuwa yakimkabili.

Taarifa kutoka Mahakamani hapo zimeeleza kuwa Diddy amepatikana na hatia katika tuhuma za kufanya usafirishaji unaohusiana na biashara ya ukahaba huku akifutiwa mashtaka mazito zaidi yaliyokuwa yakimkabili katika kesi hiyo ambayo yanahusiana na kuwalazimisha Wanawake kufanya ngono na wanaume wengine ambao walilipwa.

Hata hivyo baada ya uamuzi huo kutolewa mawakili wa Diddy waliwasilisha ombi la dhamana wakitoa kiasi cha dola milioni 1 lakini mahakama ilikataa ombi hilo huku hukumu rasmi ikitarajiwa kutolewa Oktoba 3,2025.

Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn. Kesi yake ilianza kusikilizwa Mei 5,2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags