Hailey ayavaa majukumu ya Justin Bieber

Hailey ayavaa majukumu ya Justin Bieber

Mke wa mwanamuziki kutokea Marekani Justin Bieber, Hailey Bieber ameamua kuanza kuyavaa majukumu baada ya mumewe kushuka kiuchumi na kupata changamoto za kiafya.

Taarifa hiyo imetolewa na mtu wa karibu wa familia ya Justin Bieber ambapo walifunguka kupitia gazeti la "In Touch Weekly" kwamba Hailey ambae ni mke wa Bieber ameamua kuchukua majukumu ya kazi ya Justin Bieber baada ya kupitia changamoto za kifedha na afya.


"Hailey ana ufahamu wa ajabu wa biashara na jicho halisi la mitindo," alisema mtu wa ndani.

Chanzo hicho kililiambia gazeti hilo, "Hailey pia ni shabiki nambari 1 wa Justin na anaamini kwa dhati kuwa yeye ndiye msanii bora zaidi ulimwenguni."

"Justin anapojidharau, Hailey hufanya usaidizi kwake ambao huleta maajabu na kurudisha kujiamini kwa Bieber," alisema mtu wa ndani.

Mapema mwezi Oktoba, ripoti ya gazeti la The Sun ilifichua kuwa Justin Bieber alilipishwa ushuru wa $380,000 ambayo alikuwa anadaiwa.


Hata hivyo, Hailey bado anaimani kubwa kwenye uwezo wa Justin Bieber anaamini anga ndio kikomo kwa Justin na anatamani amuinue na kumshika mkono kama vile Jay Z alivyomshika Beyonce

"Hiyo ndiyo aina ya jukumu la kimkakati ambalo Hailey ameamua kuchukua kwa Justin," amesema mtu wa ndani.

Chanzo hicho kilisema, "Hailey anavutiwa sana na ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii huwa anaconnect na mashabiki wa Justin Bieber na kuwauliza wanachotaka kutoka kwa msanii wao kitu ambacho ni muhimu sana linapokuja suala la biashara ya muziki," amesema mtu wa ndani.


Hata hivyo chanzo hicho kimeeleza kwamba Hailey kwa kawaida amekuwa ni mwenye wasiwasi zaidi na watu haruhusu mtu yeyote kumbeza au kumkashifu Justin.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags