Baada ya kuwepo kwa sintofahamu katika ndoa ya mwanamuziki Juma Jux na mke wake Pricy akidaiwa kufunga ndoa ya Kikristo na Kiislam hatimaye msanii huyo ameweka wazi kuhusiana na suala hilo.
Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari nchini Jux ameeleza kuwa alifunga ndoa moja tuu ‘Nikka’ ambayo aliifunga Ferbruari 7,2025 lakini nyingine zote hazikuwa za kweli.
“Mimi na mke wangu harusi yetu ya ukweli kabisa ni Nikka kwa sababu hata yeye kabadilisha dini sasa hivi jina lake ni Hadiza sio Pricy, na hata anniversary yetu itakuwa Februari 7 baada ya hapo tukafanya ndoa ya kiserikali kwa sababu ya makaratasi.
Yeye anakuja kuishi Tanzania inabidi apate utambulisho kwahiyo tukafanya harusi hiyo ili tutambulike kiserikali kwamba hawa ni mtu na mke wake ki-Mungu na kidini tulifunga ya Kiisilam. Kwa utamaduni wao inabidi tufanya harusi kitamaduni,”amesema Jux
Aidha ameendelea kwa kueleza “Lakini wakati tunaenda kule familia yake ni ya Wakristo na mama yake ni mtu wa Imani sana kwahiyo aliniomba sawa mshafunga ndoa na tayari ni muislam mimi kama mzazi wakati nakukabidhi mtoto wangu naomba nifanye kama kuwapa Baraka tuu na ndio maana hatukwenda kanisani. Kumleta Pasta awaombee tuu mimi nikamwambia sawa kwahiyo ile ya Nigeria ilikuwa ni kwa ajili ya kuombewa na kubarikiwa,”
Mbali na hilo msanii huyo ameweka wazi kuwa sherehe zake za harusi kuanzia Tanzania hadi Nigeria zilitumia pesa nyingi sana lakini bado hajakaa na kupiga hesabu ni kiasi gani alitumia, huku akifunguka gharama ya pete ya mkewe kuwa ni Dola 50,000 ikiwa ni sawa na Sh133 milioni.
Utofauti waPricy na wanawake wengine
“Ni jinsi mimi anavyo nitreat jinsi nikitokea sehemu anavyonihendo sijawahi kuona hilo kabla, kwao kule ni kawaida. Awali heshima nilikuwa napewa lakini kwake ananitreat like a king, nimegundua kuwa bila ruksa yangu kuna vitu vyake haviwezi kwenda.
Nafikiri wamelelewa hivyo kwao kutokana na Nigeria sehemu nyingi kuwepo na machief. Ukitaka kufanya naye jambo lazima aniulize mimi kwangu ni kama mtu wa mwisho kwenye maamuzi yake, kwahiyo hilo kwangu naona kama heshima,” amesema
Ukaribisho alioupokea baada ya kwenda Nigeria
“Nilivyoenda kufanya Bithday yangu Nigeria Mwaka jana nilimwambia tuu nataka kuja kumuona mama kawaida, kumbe yeye alikuwa ameshawaambia watu kwamba Juma anakuja mama yake na familia washani-google yaani walishanichunguza kila kitu.
Kwahiyo nilivyofika pale nikajua tunaenda tu kumsalimia mama kusema ukweli sikuwa najua chochote nafika pale nakuta mashangazi nimetandikiwa matenge chini ndio maana hata ukiangalia video zile unaona kabisa nilikuwa nashangaa. Mara ya kwanza nakutana na mama yake aliniambia sijui kitu kukuhusu lakini nadhani wewe ni mtu mzuri,”amesema Jux

Leave a Reply