Kitundu azikwa makaburi ya Wailes

Kitundu azikwa makaburi ya Wailes

Mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa Jua Kali Raidanus Vitalis 'Kitundu' umezikwa leo Juni 26, 2025, katika makaburi ya Wailes, Temeke.


Kitundu alifariki dunia Jumanne jioni, Juni 24, 2025, katika hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya tumbo na kifua, kama alivyobainisha baba yake mdogo.

Taarifa za msiba huo zilitolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa mzalishaji na mwongozaji wa tamthilia aliyokuwa akiigiza ya ‘Jua Kali’, Leah Mwendamseka 'Lamata.'



Enzi za uhai wake, Kitundu aliigiza kwenye tamthilia hiyo kama kijana mwenye kipaji cha kucheza muziki anayetokea kwenye familia ya kimasikini. Kisha baadaye anapata nafasi ya kutoboa kimaisha lakini anashindwa kuitumia vizuri na kujikuta akirudi kwenye maisha ya kimasikini.

Aidha enzi za uhai wake marehemu Kitundu alijihusisha na masuala ya Udensa ambapo alifanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi kamavile Vanessa Mdee, Chino Kidd, Sumalee, nawengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags