Kisa cha Beyonce kuzabwa makofi na mama yake

Kisa cha Beyonce kuzabwa makofi na mama yake

Peter Akaro

Mwimbaji Beyonce katika kitabu chake, Become Beyonce: The Untold Story (2015) amefichua jinsi mama yake mzazi, Tina Knowles alivyokomesha mara moja mahusiano yake na mvulana, Lyndall Lock wakati akiwa na umri wa miaka 15.

J Randy ambaye ni mwandishi wa kitabu hicho chenye kurasa 451, anadai ukali wa Tina ulimfanya Lyndall kukaa mbali kabisa na Beyonce licha ya kuwa walikuwa wanasali kanisa moja.

Mama huyu alikuwa mkali kwa Beyonce hata alipofikisha miaka 18, hata alipoanza ukaribu na Jay Z, yeye ndio aliamua kama wanaweza kutoka kwenda matembezi au laa.

Beyonce anaeleza hawezi kusahau tukio la kuzabwa makofi na mama yake hadharani katika duka wakati akiwa na umri wa miaka 19, tayari alikuwa msanii maarufu wa kundi la Destiny's Child.

Mwimbaji wa kibao, Dangerously in Love (2003), alikula makofi hayo kutokana alikuwa akiwaimbia wanaume waliomvutia dunikani hapo wakati mama yake anamuongelesha na yeye kutojali hilo.

Hilo lilimfanya kuelewa kuwa alianza kupotea taratibu kitabia na ikambidi kujirekebisha ingawa mwenyewe anadai alikuwa na aibu sana mbele za wanaume kwa kipindi hicho.

Baada ya Destiny's Child kuachia albamu yao ya pili, The Wrinting's on the Wall (1999), wasanii wawili, LeToya Luckett na Roberson waliachana na kundi hilo jambo lilompa msongo wa mawazo Beyonce.

Lakini mama yake licha ya ukali ndiye alikuwa mfariji wake wake mkuu kutokana alishindwa kuzungumzia hilo kwa sababu ndipo tu walikuwa wameshinda tuzo ya Grammy.

Kwa ujumla Destiny's Child waliovuma na nyimbo kama Bills, Bills, Bills (1999) na Survior (2001), waliwania Grammy mara 14 na kushinda mara tatu ambapo mwaka 2001 walishinda mbili kufuatia kufanya vizuri kwa wimbo wao, Say My Name (1999).

Ikumbukwe Tina aliolewa mwaka 1980 na Mathew Knowles ambaye alikuwa ni meneja wa Destiny's Child, katika ndoa yao walijaliwa watoto wawili ambao ni Beyonce (1981) na Solange (1985), kabla ya kutalikiana mwaka 2011.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags