Mkali wa Pop kutoka Marekani, Madonna amemuomba Papa Leo XIV, akimsihi kwenda Gaza ili kuwasaidia watoto wanaoteseka kutokana na mgogoro unaoendelea.
Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii Agosti 12, 2025, nyota huyo amesisitiza kuchukuliwa hatua za dharura ili kukabiliana madhira kwa watoto kutokanana vita vinayoendelea baina ya Palestina na Israel eneo la Gaza.
Katika ujumbe huo aliomwandikia Papa Leo XIV, Madonna ameandika: “Baba Mtakatifu, nakusihi utembelee Gaza na kuangazia maisha ya watoto kabla hali haijawa mbaya zaidi. Mimi kama mama, siwezi kuvumilia kushuhudia mateso yao. Watoto wa dunia ni jukumu letu sote.”
Modana amesema kwamba Papa Leo wa XIV yupo kwenye nafasi ambayo anaweza kuingia Gaza, akisema: “Wewe ndiye pekee kati yetu ambaye huwezi kunyimwa kuingia.”
Madonna ametoa wito wa kuondolewa vikwazo kwa lengo la kuruhusu kupelewa misaada mbalimbali ya kibinadamu ili kuokoa maisha ya wasio na hatia.
Papa Leo wa XIV mara kwa mara ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano Gaza na kuhimiza kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu. Katika matamko yake ya karibuni, amelaani mateso ya raia, hususan watoto na amepinga adhabu za pamoja na kuwaondoa watu kwa nguvu.

Leave a Reply