Mfahamu Jenny Joseph Wa Columbia Pictures

Mfahamu Jenny Joseph Wa Columbia Pictures

Kama umekuwa ukijiuliza maswali kuhusu mwanadada anayeonekana mwanzoni mwa filamu nyingi za ‘Columbia Picture’ basi haya ndio majibu halisi kuhusu mwanamke huyo.

Jina lake ni Jenny Joseph alikuwa akifanya kazi katika moja ya kampuni ya magazeti. Akiwa hana wazo lolote kwamba picha yake ingetazamwa na mamilioni ya watu duniani alipigwa picha hiyo wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana.

Tukio hilo lilitokea mwaka 1992 Jenny akiwa designer katika gazeti la The Times-Picayune huko New Orleans, Marekani. Alitoka na marafiki zake wakati wa chakula cha mchana ambapo nje ya ofisi alikutana na mtu ambaye alimuomba kushiriki kupiga picha ya kisanii hivyo basi alikubali bila kujua picha hiyo ingekuwa alama kubwa.

Michael Deas, ambaye alikuwa mchoraji alipewa kazi ya kuboresha nembo ya ‘Columbia Pictures’ ambapo macho yake yaliridhika kufanya kazi na Jenny. Kwa kuwa mwanadada huyo aliona ni tukio la kawaida alikubali kuwa model japo hakuwa mtaalamu wa mitindo.

Baada ya picha hiyo kupingwa Michael Deas aliihariri na kuonekana kama katuni kiasi kwamba watu wengi hawakujua kuwa alikuwa Jenny mpaka pale Deas alipofichua kwenye moja ya mahojiano yake akieleza kuwa Jenny Joseph ndiye model aliyepiga picha ya awali iliyomsaidia kuunda mchoro wa "Torch Lady" wa Columbia Pictures mwaka 1992.

Licha ya sura yake kuwa nembo ya kampuni kubwa ya filamu duniani. Hakuwa maarufu kwa jina lake halisi wala hakufaidika moja kwa moja kifedha kwa matumizi ya picha hiyo iliyotumika kwa mara ya kwanza mwaka 1993 kwenye filamu za kampuni hiyo.

Inaelezwa mwanadada huyo alipokea malipo siku ile ile ambayo alipiga picha na kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali alipokea malipo ya kawaida sana na sio makubaliano ya kibiashara. Hata hivyo, Columbia Pictures haikutangaza jina lake hadharani kwa muda mrefu na hakuwa sehemu ya mikataba wala promosheni za baadaye.

Jenny Joseph ambaye alizaliwa Mei 7, 1932 huko Birmingham, Uingereza alianza kupata umaarufu baada ya kutoa vitabu vyake vya mashairi kikiwemo cha Warning na Rose in the Afternoon ambavyo vilipelekea kushinda tuzo mwaka 1986 ya James Tait Black Memorial Prize kwa riwaya yake Persephone. Na mwaka 1995 alipata Forward Prize kwa mkusanyiko wake wa mashairi.

Jenny aliishi Gloucestershire, Uingereza, mpaka pale umauti ulipomfika ambapo alifariki dunia Januari 8, 2018 akiwa na umri wa miaka 85. Aliolewa na Charles (Tony) Coles, ambaye walifunga ndoa mwaka 1961 na walifanikiwa kupata watoto watatu.

Sura ya Jenny kupitia mchoro wa "Torch Lady" wa Columbia Pictures imeonekana kwa zaidi ya filamu 1000 tangu ilipoanza kutumika rasmi mwaka 1993 ikiwemo Men in Black, Spider-Man, The Pursuit of Happyness, Jumanji na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags