Mwigizaji kutoka Marekani ambaye amekuwa akihusishwa kwenye kesi za Diddy, Michael B. Jordan ameripotiwa kuwa hatotoa ushahidi katika kesi hiyo ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara za kingono.
Kwa mujibu wa jarida la People, wakati majaji wapya wakipewa maelekezo kuhisana na kesi hiyo walielezwa mchakato mzima pamoja na kutaja majina ya mastaa wakiwemo Casandra “Cassie” Ventura, Kanye West, Mike Myers, na Kid Cudi.
Huku katika orodha hiyo jina la Jordan likitajwa kutokana na uhusiano wake na mpenzi wa zamani wa Combs, Ventura, hivyo basi kutokana na hilo hatotoa ushahidi mahakamani. “Michael Jordan hatakuwa shahidi katika kesi hiyo,” chanzo kimoja kiliiambia People.
Utakumbuka wakati mwanadada Cassie akiwasilisha kesi yake mahakamani alieleza kuwa mwaka 2015 alianza uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Jordan na mara baada ya Combs kugundua kuhusu uhusiano huo alimwita mwigizaji huyo na kumtishia.
Katika kesi hiyo ya Diddy mambo bado ni magumu kwani baada ya Combs kuulizwa kuhusiana na tuhuma zianazomkabili msanii huyo alikataa jambo ambalo lilipelekea jaji mkuu kutafuta majaji wengine watakao saidia kuchunguka kesi hiyo.
Hivyo basi taarifa za awali na ushahidi bado haujaanza kusikilizwa lakini shauli hilo linatarajiwa kuanza kufanyiwa kazi Mei 12,2025.

Leave a Reply