Mirabaha Ya Wasanii Kuongezeka Maradufu

Mirabaha Ya Wasanii Kuongezeka Maradufu

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema kuwa katika kipindi cha Septemba 2023 hadi Novemba 2024 COSOTA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla zaidi ya shilingi bilioni moja, milioni mia moja tisini na tano na laki tano (1,195,533,072.92) ambazo zimekusanywa kupitia tozo ya hakimiliki.

Taarifa hiyo ameitoa Januari 13, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Ofisi ya Hakimilika Tanzania (COSOTA) na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) kuhusu kulipia Mirabaha kutokana na matumizi ya kazi ya muziki.

Mhe. Mwinjuma ameongeza kuwa chanzo hicho cha tozo ya hakimiliki kimekuwa chachu ya mapato ya mirabaha kuongezeka ikizingatiwa kuwa mgao uliofanywa na COSOTA Julai 2023 kwa kazi za muziki ulikuwa ni Shilingi milioni 396,947,743 na jumla ya wanufaika 8,018.

"Chanzo hiki kipya kimekusanya mapato zaidi na kitanufaisha wasanii na waandishi wa kada zote ukilinganisha na fedha iliyogawiwa kwa wasanii walionufaika mwaka 2023 katika mgao wa mwisho.

Wakati huu hata wasanii na wamiliki wa hakimiliki katika aina nyingine za kazi za Sanaa na uandishi watanufaika na mirabaha hii ambayo inategemewa kugawiwa haraka punde tu baada ya fedha hizo kupokelewa kutoka Wizara ya Fedha,”amesema Mhe Mwana FA






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags