Muziki si kitu kwenye utajiri wa Jay Z

Muziki si kitu kwenye utajiri wa Jay Z

Unaambiwa licha ya Jay-Z kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani, lakini muziki wake unachangia kwa asilimia tatu pekee kwenye utajiri wake.

Rapa na mjasiriamali huyo ni mshindi wa tuzo za Grammy mara 25, kama ilivyoripotiwa na Jarida la Forbes. Jay Z anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola 2.5 bilioni. Licha ya kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani ni asilimia tatu  tu ya utajiri wake unatokana na muziki na asilimia 97 iliyobaki inatokana na mapato mengine ya kibiashara.

Jigga aliweka historia ya kuwa rapper wa kwanza bilionea mwaka 2019, ambapo amejikusanyia utajiri wake kwa miaka mingi kupitia muziki na mfululizo wa miradi ya kibiashara iliyomfanya apate utajiri zaidi.
Jinsi biashara zinavyochangia utajiri wa Jay Z

Ukiachilia mbali kazi yake kama msanii, Jay-Z pia ni mjasiriamali na mwekezaji mkubwa kwenye miradi tofauti tofauti ya kibiashara.

Matarajio ya kufanikiwa kwa Jay-Z yalikuwa ni zaidi ya muziki, kwani rapa huyo aliingia katika ulimwengu wa mitindo ya mavazi mwaka 1999, baada ya kuzindua mavazi yake ya 'Rocawear'. Ambayo hivi karibuni yalikuja kuwa ya kitamaduni, mpaka kufikia mwaka 2007 alifanikiwa kuingiza dola 204 milioni.
 
Jay Z amefanikiwa kuanzisha kampuni nyingine nyingi ikiwa ni pamoja na za vinywaji ambazo zimemfanya aingize mkwanja mrefu zaidi. Mwaka 2014 alinunua chapa ya kwanza ya Champagne inayofahamiaka kama Arman de Brignac. Lakini pia 2021 kampuni ya kifahari ya Moët Hennessy Louis Vuitton (LVMH) ilinunua hisa ya asilimia 50% kwenye chapa hiyo na kumfanya Jay Z kuendelea kuingiza pesa ndefu zaidi.

Kwa kila chupa moja ya Champagne ya chapa hiyo inauzwa kwa dola 300 ambayo ni sawa na sh 781,500.00, ambapo rapa huyo bado anamiliki asilimia 50 iliyobaki ya chapa hiyo.

Aidha, mwaka 2023 Jay-Z alianzisha chapa yake ya pombe ya kifahari ya D'Usse, kwa mujibu wa jarida la 'Variety' liliripoti kuwa kampuni ya vinywaji ya Bacardi, ilinunua hisa nyingi za D'Usse zenye thamani ya dola 750 milioni.

Pia Jay Z ni mmiliki wa Roc Nation

Roc Nation ni kampuni ya burudani iliyoanzishwa na Jay-Z ambayo ina record lebo ya usimamizi wa vipaji vya muziki, michezo, uchapishaji, na sehemu ya usambazaji wa kazi tofauti tofauti za sanaa. Baadhi ya wasanii wakubwa ambao wapo chini ya lebo hiyo ni pamoja na Rihanna, Shakira, na Kyrie Irving wengine wengi. Lebo hiyo ina simamia wasanii zaidi ya 40.

Roc Nation imekuwa katika ushirikiano na NFL tangu mwaka 2019, kama wataalamu rasmi ambao huweka mikakati ya kiburudani hususani muziki ambao hutumbuizwa LIVE kila mwaka kwenye Half ya fainali ya ligi hiyo. Ambapo hutoa nafasi kwa wasanii mbalimbali kwa mwaka huu 2025, alichapa Kendrick Lamar, 2024 aliua Usher Ray Mond, 2023 alikuwepo Rihanna. Hii imekuwa sehemu nyingine ya Jay Z kujiingiza mpunga na heshima. Mwaka 2022, Jay-Z alishinda tuzo ya Emmy kwa utengenezaji wake wa Super Bowl Halftime Show.

Mwaka 2015, Jay-Z alinunua huduma ya kutiririsha muziki ya Tidal, kwa Dola 56 milioni kitu ambacho kilipelekea rapa huyo kuondoa muziki wake Spotify na kuuhamishia kwenye jukwaa la Tidal, hili lilikuwa ni wazo la kibiashara la kuwa na muziki wa kipekee unaopatikana kwenye platform ya Tidal.

Lakini mwaka 2021 Jay-Z aliuza hisa zake za Tidal kwa Dola 297 milioni kwa Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Twitter 'Jack Dorsey'. Na kujiunga na bodi ya wakurugenzi ya Tidal Square.

Jay Z pia naendelea kuwa tajiri kutokana na umiliki wake wa visiwa, na mkusanyiko wa mali nyingi huko New York na Los Angeles.

Jay-Z na Beyoncé wanamiliki mali za mamilioni ya dola zikiwemo nyumba za kifahari mwaka 2023, wanandoa hao walinunua nyumba ya gharama kubwa zaidi kuwahi kuuzwa ambalo walinunua kwa dola 200 milioni, huko California eneo lake ni sawa na futi za mraba 40,000 Jay-Z pia anamiliki mali huko East Hampton, New York, na upenu huko Tribeca.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags