
Ndoa Ya Govinda Na Mkewe Ipo Matatani
Baada ya kudumu katika ndoa kwa takribani miaka 37, mwigizaji mkongwe wa Bollywood, Govinda Arun Ahuja na mke wake Sunita Ahuja, wameripotiwa kuachana huku sababu ikidaiwa kuwa Govinda ana mahusiano mengine.
Kwa mujibu wa Zoom TV, Govinda na mke wake Sunita wamekuwa wakiishi sehemu tofauti kwa muda mrefu na sasa wanatarajia kupeana talaka baada ya kudumu kwa miaka 37 kwenye ndoa yao.
Ingawa mwigizaji huyo wa Bollywood na mkewe bado hawajathibitisha hilo lakini chanzo cha karibu cha familia hiyo kinadai, mwigizaji katika filamu ya Partner mwenye umri wa miaka 30 ndio sababu ya talaka ya wawili hao.
Govinda amekuwa katika ndoa na Sunita Ahuja tangu mwaka 1987, na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni binti aitwaye Tina (Narmada) na mvulana, Yashvardhan.
Leave a Reply