Ni Kweli Kapendeza Kuliko Wote Kwenye Met Gala

Ni Kweli Kapendeza Kuliko Wote Kwenye Met Gala

Diljit Dosanjh mwanamuziki na mwigizaji kutoka Punjab, naye alihudhuria kwa mara ya kwanza katika Met Gala 2025, huku vazi lake likitajwa kuwa vazi bora kuwahi kutokea katika maonyesho hayo.

Katika mitandao ya kijamii mashabiki na wadau mbalimbali walilisifia vazi la Diljit lililotawaliwa na rangi nyeupe huku wengi wao wakilitaja kuwa vazi bora kuwahi kutokea kwenye Met Gala.

Ingawa hakuweka wazi jina la mbunifu wa vazi lake, ripoti zinaonyesha kuwa alivalia vazi la kipekee lililobuniwa na Prabal Gurung, mbunifu maarufu ambaye pia alibuni vazi la Alia Bhatt kwa ajili ya Met Gala ya mwaka 2024.



Ushiriki wa Diljit katika Met Gala 2025 unaashiria hatua kubwa katika safari yake ya kimataifa, baada ya mafanikio yake katika matukio kama Coachella na Paris Fashion Week. Kwa mashabiki wake, hili ni tukio la fahari linaloonyesha jinsi wasanii wa India wanavyoendelea kung'ara katika majukwaa ya kimataifa.

Mbali na kuoneaka kimataifa lakini msanii huyo aliwahi kufanya kolabo na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond wakiachia ngoma iitwayo ‘Jugni’ iliyotoka mwaka 2022 huku ikitazamwa zaidi ya mara milioni 29 katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags