Walio nyuma ya tamasha lililomponza Andy Byron

Walio nyuma ya tamasha lililomponza Andy Byron

Siku kadhaa zilizopita ilizuka sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii baada ya Andy Byron, ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Astronomer Inc. ya nchini Marekani kunaswa na kamera akikumbatiana na mwanamke ambaye hakuwa mkewe, kwenye tamasha la muziki la Coldplay. Lifahamu zaidi tamasha hilo na walio nyuma yake.

Tamasha hilo ambalo hadi sasa bado linaendelea, linafanywa na Coldplay ambao ni bendi ya muziki wa rock kutoka Uingereza, iliyoanzishwa London mwaka 1997. Bendi hiyo ilianzishwa na Chris Martin na Jonny Buckland walipokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha London (UCL).

Kisha baadaye walijiunga na Guy Berryman na Will Champion, na hatimaye wakampata Phil Harvey kama meneja wao. Awali, waliitambulisha bendi hiyo kwa jina la Pectoralz, kisha Starfish, kabla ya kubadilisha jina rasmi na kuwa Coldplay mwaka 1998.

Baadhi ya albamu za bendi hiyo ni Parachutes (2000), 'A Rush of Blood to the Head (2002), X\&Y (2005), Viva la Vida or Death and All His Friends (2008), na nyinginezo huku wimbo wa Viva la Vida ukiongoza chati za muziki duniani na kuwa wimbo wao wa kwanza kuongoza kwenye chati ya Billboard Hot 100 nchini Marekani.

Mbali na hayo kawaida bendi hiyo huwa na ziara mbalimbali ambazo moja wapo ni hii ya Music of the Spheres iliyowaibua wawili hao waliokuwa wakikumbatiana.

Music of the Spheres ni ziara yao nane iliyoanza rasmi Machi 18, 2022 ikasimama kwa sababu ya janga la COVOD 19. Sasa inaendelea hadi Septemba 8,2025. Huku kati ya sababu za kufanya ziara hii ni kutangaza albamu yao ya tisa na ya kumi, ambazo ni Music of the Spheres (2021) na Moon Music (2024).

Hivyo basi wakiwa katika tamasha hilo ndipo mambo yaligeuka kwa Kristin Cabot na Andy Byron baada ya kamera kuwanasa na video zao kuanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu Jumatano ya wiki iliyopita.

Utakumbuka kipindi waliponaswa na kugundua kuwa walikuwa wakionyeshwa kwenye skrini kubwa ndani ya uwanja wa Gillette wakati wakikumbatiana, Byron alijificha na Cabot alifunika uso wake kwa mikono. Hadi sasa tayari Andy Byron anadaiwa kuachia ngazi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags