Hamilton atangaza kutumia jina la mama yake

Hamilton atangaza kutumia jina la mama yake

Moja ya story za kimataifa zinazobamba huko mitandaoni ni hii ya bingwa mara saba wa mbio za magari ya Formula 1, Lewis Hamilton kutangaza kubadilisha jina la ukoo wake kwa kuongeza jina la mama yake mzazi.

Hamilton ametangaza kubadilisha jina hilo la ukoo na kutumia jina la mama yake mzazi kwa sababu kwamba haelewi kwanini mwanamke hupoteza jina lake akiolewa.

Lewis Hamilton aliishi na mama yake Carmen Larbalestier mpaka alipofikisha miaka 12 na kuchukuliwa na baba yake.

Pia imeelezwa kuwa Hamilton amefanya hivyo kwa heshima ya mama yake mzazi Carmen Larbalestier ambaye alitengana na baba yake Anthony Hamilton tangu akiwa na umri wa miaka miwili.

Kutengana kwa wazazi hao kulimfanya Hamilton kulelewa na mama yake mpaka alipofikisha miaka 12 alipohamia kwa baba yake ambaye alikuwa ameoa mwanamke mwingine na kupata watoto wawili.

Kwa sasa Lewis anataka kutambulika kwa jina la Lewis Carl Davidson Larbalestier Hamilton.

''Kwa sababu sielewi kabisa wazo zima la kwanini, watu wanapooana, mwanamke hupoteza jina lake. Nataka jina lake liendelee na jina la Hamilton." amesema Lewis Hamilton.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags