Kipande cha video hiyo kimenaswa katika filamu ya kumbukumbu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni iliyopewa jina la ‘In Whose Name?,’ ambacho kilipostiwa jana Jumatano kwenye Youtube kikiwaonesha wawili hao wakiwa wamekaa pamoja huku Kim akionesha hisia zake kwa Kanye akimwambia kuwa season amebadilika sana.

“Tabia yako haikuwa hivi miaka michache iliyopita! Sielewi kilichompata yule mwanaume niliyemfahamu. Umebadilika sana, na ni kama nazungumza na mtu tofauti kabisa na yule niliyempenda,”alisikika akisema Kim kwenye video hiyo.
Mbali na kipande hicho kuwavuruga wengi lakini pia kulikuwepo na vipande vingine ikiwa ni pamoja na maisha yake akiwa na watoto wake North, Saint, Chicago na Psalm, kazi zake za kimuziki, mtindo wa mavazi, nyakazi za maombi na nyimbo Sunday Service pamoja na matukio makubwa likiwemo Tamasha la Coachella mwaka 2019.
Filamu hiyo ambayo imeongozwa na Nico Ballesteros, ilirekodiwa wakati alipokuwa akimfuatilia Kanye kwa zaidi ya miaka sita akirekodi maisha yake ya hadharani na binafsi, filamu hiyo inatajwa kufichua namna rapa huyo alivyopanda kutoka kuwa msanii maarufu hadi kuwa mtu mmoja wa watu weusi matajiri zaidi Marekani.
Filamu hiyo inatarajiwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Septemba 19,2025 katika maelfu ya kumbi za sinema za AMC nchini Marekani.
Kim Kardashian na Kanye West walifunga ndoa Mei 24, 2014 sherehe ambayo ilikuwa ya kifahari iliyofanyika Florence, Italia. Ndoa yao ilihudhuriwa na familia, marafiki wa karibu, na watu mashuhuri mbalimbali, huku mahusiano yao yakifuatiliwa zaidi na vyombo vya habari duniani kote.
Wakati wa ndoa yao, walijaaliwa kupata watoto wanne, North (2013), Saint (2015), Chicago (2018), na Psalm (2019). Mwaka 2021 Kim aliwasilisha ombo la talaka mahakamani na hatimaye alifanikiwa kupata talaka yake Novemba 2022.
Sababu kuu za kuachana kwao, kulingana na ripoti na mahojiano ya baadaye, ilihusiana na tofauti kubwa za kimaisha na changamoto za kiafya za akili alizopitia Kanye, hasa baada ya kutangaza hadharani kwamba ana ugonjwa wa bipolar.
Bipolar ni ugonjwa wa akili unaosababisha mabadiliko makubwa ya hisia, ambapo mtu hupitia vipindi vya furaha na nguvu kupita kiasi (mania) na kisha vipindi vya huzuni au kukata tamaa (depression).
Leave a Reply