Mwanamke anayemtuhumu nyota wa muziki Jay-Z, kumfanyia unyanyasaji wa kingono akiwa na miaka 13, mwaka 2000, ameendelea kufichwa utambulisho wake na mahakama.
Analisa Torres ambaye ni hakimu wa kesi hiyo amesema mwanamke huyo halazimiki kufichua utambulisho wake kwani sheria za mahakama zinamruhusu kufanya hivyo.
"Uwasilishaji wa mara kwa mara wa wakili wa Carter 'Jay-Z' wenye hoja za kupinga zenye lugha ya uchochezi na mashambulizi haufai, ni upotevu wa rasilimali za mahakama, na mbinu ambayo haiwezi kumnufaisha mteja wake," aliandika Jaji Torres katika uamuzi wake, kulingana na hati za mahakama zilizoripotiwa na jarida la PEOPLE.
Hata hivyo mwanamke huyo, ambaye aliwasilisha kesi yake kwa jina bandia la Jane Doe, alidai kufanyiwa vitendo hivyo baada ya hafla za ugawaji wa Tuzo za Muziki za MTV miaka 24 iliyopita. Awali alimshtaki Diddy mnamo Oktoba, na miezi miwili baadaye akarekebisha malalamiko yake, na kumuongeza Jay-Z kwenye madai hayo.
Utakumbuka mwanasheria wa Jay-Z alisema jalada la mteja wake kulalamikiwa linapaswa kutupiliwa mbali ikiwa mtoa mashtaka hatafichua utambulisho wake lakini.
Leave a Reply