Manara apata ajali

Manara apata ajali

Moja kati ya story zinazobamba katika mitandao ya kijamii ni ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya gari usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Manara kupitia akaunti yake ya Instagram amekiri kupata ajali hiyo ambapo amesema amenusurika kwenye ajali hilo ambayo imeliacha gari yake ikiwa imeharibika vibaya.

Msemaji huyo amefunguka hayo wakati akielezea sababu zilizomfanya ashindwe kufika kwenye mahojiano na kituo cha Radio cha Efm Leo saa 12 asubuhi.

“Usiku wa kuamkia jana nilinusurika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kiaribika vibaya. Nawaomba radhi sana nyie wasikilizaji na watazamaji wote mnisamehe sana na nimejisikia vibaya sana” amesema Manara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags