Mapacha tisa waliozaliwa kwa wakati mmoja  wamerejea salama nchini kwao

Mapacha tisa waliozaliwa kwa wakati mmoja wamerejea salama nchini kwao

Mapacha tisa pekee duniani - watoto waliozaliwa kwa wakati mmoja - wamerejea salama nchini kwao Mali.

Wazazi na watoto hao tisa waliwasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu, Bamako, Jumanne na kukaribishwa na Waziri wa Afya Diéminatou Sangaré.

Walikuwa wakiishi katika eneo la matibabu huko Casablanca Morocco tangu waondoke katika zahanati ya Ain Borja ambapo watoto hao walizaliwa tarehe 4 Mei 2021.

Watoto hao walivunja rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi waliozaliwa wakati mmoja na kuishi.

Watoto hao - wasichana watano na wavulana wanne - walitungwa mimba kwa kutumia matibabu ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi (IVF) na walizaliwa kwa upasuaji.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags