Nguli Wa Mieleka Hulk Hogan Afariki Dunia

Nguli Wa Mieleka Hulk Hogan Afariki Dunia

Mwanamieleka maarufu ambaye amewahi kutamba katika shirika la mieleka WWE, Hulk Hogan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71.

Taarifa za kifo chake zinaeleza kuwa Hogan ambaye jina lake halisi ni Terry Gene Bollea amefariki alfajiri ya leo Julai 24,2025 akiwa nyumbani kwake Clearwater, Florida, nchini Marekani baada ya kupata mshituko wa moyo.

Hata hivyo polisi jijini Clearwater wamesema alikimbizwa hospitalini lakini alitangazwa amefariki muda mfupi baadaye.

Katika maisha yake ya ulingo, Hogan alipata mataji mengi ya mieleka likiwemo WWF World Heavyweight Championship akishinda mara 6 lakini pia alionekana katika filamu na vipindi vya televisheni, akiwahamasisha mashabiki wa michezo hiyo duniani kote.

Enzi ya uhai wake Hulk Hogan amewahi kupambana na wanamieleka maarufu sana katika historia ya mieleka ya kulipwa akiwemo André the Giant, The Ultimate Warrior, "Macho Man" Randy Savage, The Rock, Triple H, Kurt Angle, Brock Lesnar, The Undertaker nk.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags