Wengi wanamfahamu Tyla kwa ngoma zake za kuvutia ikiwemo ‘Water’, lakini mashabiki wengi hawajui kuwa nyota huyo ambaye sauti yake inaushawishi mkubwa katika jamii kuwa anacho kipaji kingine cha kuchora.
Kufuatia na video yake aliyoshare katika mtandao wake wa instgarma, Tyla alifichua kuwa yeye ndiye aliyechora picha zote ambazo zimeonekana kwenye moja ya video ya wimbo wake wa ‘Art’ jambo ambalo liliwashangaza mashabiki wengi.
Katika video hiyo Tyla alisema kuwa ndiyo aliyechora picha hiyo mwenyewe akiwa nyumbani kwake akiweka wazi kuwa hiyo ni sehemu ya kujituliza kimawazo na kihisia anapokuwa mbali na mambo ya kimuziki.
Aidha, kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa msanii huyo amepanga kupeleka picha zake katika maonesho ya kisanaa siku zijazo, jambo ambalo litamuwezesha kuchanganya vipaji vyake vyote kwa wakati mmoja.
Katika wimbo huo Tyla ameweka picha mbalimbali zikiwemo ambazo amezichora miezi michache iliyopita nyingine zikiwa zile ambazo amezichora wakati yupo shule ya msingi na chuo.
Tyla amejizolea umaarufu kupitia ngoma zake ambazo zilifanikiwa kuingia katika chati ya Billboard Afrobeats ikiwemo Water, Truth or Dare, Jump, ART na nyinginezo.

Leave a Reply