Morgan Freeman ni jina kubwa katika tasnia ya filamu duniani. Amejizolea heshima na upendo kwa jamii kufuatia na uigizaji wake wa kipekee pamoja na uwezo wake wa kuigia kwenye kila uhusika anaopewa.
Lakini kwa wengi wetu tunamjua kama mzee mwenye busara, mwenye mvi nyingi na tabasamu la utulivu, hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezuka swali likiuliza mashabiki kama wamewahi kumuona Morgan Freeman akipwa kijana?.
Swali hilo limezua mijadala huku wengi wao wakieleza kuwa hawajawahi kumuona akiwa kijana, hata hivyo baadhi ya tovuti zinaeleza kuwa mwigizaji huyo alichelewa kupata umaarufu kwani enzi ya ujana wake alitumia kujitafuta katika tasnia ya burudani.
Freeman alizaliwa mwaka 1937 Memphis, Tennessee, Marekani. Alianza kuigiza akiwa na umri mdogo, lakini mafanikio makubwa katika filamu hayakumfikia haraka. Miaka ya 1960 hadi 70, alikuwa akiigiza kwenye michezo ya jukwaani na vipindi vya watoto kwenye televisheni kama The Electric Company.
Wakati huo, alikuwa kijana mwembamba mwenye uso wa matumaini, nywele nyingi nyeusi akiwa mbali sana na sura ya hekima tunayoiona leo kwenye filamu kama The Shawshank Redemption, Bruce Almighty, Invictus na nyinginezo.
Hata hivyo leo hii, akiwa na zaidi ya miaka 80, bado anafanya kazi, akithibitisha kuwa umri si kikwazo cha mafanikio.

Leave a Reply