Punda Wa Kwenye Katuni Ya Shrek, Afariki Dunia

Punda Wa Kwenye Katuni Ya Shrek, Afariki Dunia

Punda liyejizolea umaarufu kupitia filamu ya katuni ya ‘Shrek’ aliyepewa jina la Perry amefariki dunia akiwa na miaka 30.

Taarifa ya kifo chake ilithibitishwa na hifadhi ya wanyama kutoka San Francisco Bay iitwayo ‘Barron Park Donkey Project’ ikiweka wazi kuwa mnyama huyo aliaga dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mifupa na misuli kwa muda mrefu.

Perry, punda mdogo wa aina ya Jerusalem, alizaliwa New York mwaka 1994 na ilipofikia mwkaa 1997 Punda huyo alihamishiwa San Francisco Bay kwa uangalizi mzuri zaidi.

Punda ‘Perry’ alijizoeleza umaarufu kupitia filamu ya katuni ya ‘Shrek’ huku uhusiaka wake ukiwaburudisha watu kupitia sauti ya Eddie Murphy, filamu hiyo iliachiwa rasmi April 2001 ikiongozwa na Andrew Adamson na Vicky Jenson.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags