Rihanna akisrishwa na akili bandia kutumia sauti yake

Rihanna akisrishwa na akili bandia kutumia sauti yake

Staa wa muziki na mjasiriamali Rihanna, amejitokeza kukanusha video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akizungumza kuhusu manunuzi yake ya vitu vya gharama kubwa.

Video hiyo, ambayo ilitumia akili bandia 'AI' na kuiga sauti yake, haikuwekwa wazi kuwa ni sauti ya AI, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuhoji uhalisia wake.

Rihanna mwenyewe alitoa maoni yake kwenye video hiyo akionyesha kushangazwa baada yakuandika ,“Who tf is this talking??!”.

Aidha, mashabiki wake pia walionyesha mashaka yao juu ya sauti hiyo wakisema Rihanna wa kweli hawezi kujisifu kwa mali zake.

Utakumbuka kuwa hii si mara ya kwanza sauti ya msanii huyo kutumiwa na akili bandia bila ruhusa yake kwani mwaka 2023, wimbo bandia wa Rihanna na BadBunny ulisambaa kwenye SoundCloud, kama ilivyotokea kwa wimbo wa AI wa Drake na TheWeeknd.

Hata hivyo, mashabiki wa Rihanna wataweza kumsikia kwa sauti yake halisi kwenye filamu mpya ya Smurfs, ambapo atacheza kama Smurfette ambapo Trela ya filamu hiyo, inayotarajiwa kutoka Julai mwaka huu imeshatolewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags