Tory Lanez amtaka Rick Ross ampatie gari alilomuahidi

Tory Lanez amtaka Rick Ross ampatie gari alilomuahidi

Unaambiwa unapoahidi jambo bwana basi  hakikisha unalitimiza kwani siku zote ahadi ni deni, hili limemkuta Rapa Rick Ross ambaye alimuahidi Rapa mwenzie Tory Lanez zawadi ya gari mwaka jana.

Tory Lanez baada ya kuona muda unakwenda bila kupatiwa gari hilo ameamua kumkumbusha Kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuandika hivi.

Rozay lile gari mbona hunipatii”……Nadhani alifikiri kuwa sote tuna mkwanja mrefu ndio maana alijua kwamba sitoulizia… Gari langu liko wapi Rick..??”aandika ToreyLanez

Rozay alithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa instagram kwenye insta-story yake mwaka jana kuwa amemnunulia Gari Rapa huyo na hivyo atampatia zawadi yake.

Ebwana eeh comment hapo chini jamaa alikua na haja ya kumdai mshikaji au angekausha tu?! Tuambie.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags