Kampuni ya Apple imetoa mwongozo mpya wa usalama ukionya wamiliki wa iPhone kuepuka kuchaji simu zao kwenye mashuka, mito na godoro (kitandani).
Kwa mujibu wa Apple, betri za simu za kisasa aina ya ‘lithium-ion’ hupata moto sana wakati wa kuchaji hivyo simu ikiwekwa juu ya kitanda au mto hewa ya kupooza joto haiwezi kupita vizuri na joto kuongezea na kufikia kiwango cha hatari.
Ambapo matokeo yake, simu inaweza kuungua na hata kusababisha moto mkubwa unaoweza kuharibu mali au kumuunguza mtu anayelala karibu na simu inayochajiwa.
Hata hivyo ushauri wa wataalamu umetoa miongozwa ambayo ni kuweka mbali simu inayochajiwa katika kitu kigumu na tambarare kama Meza au Kabati, kuhakikisha kuna nafasi ya kupita hewa, epuka kufunika simu kwa blanketi au nguo wakati wa kuchaji na Tumia chaja na nyaya za asili au zenye ubora unaokubalika.

Leave a Reply