Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Burna Boy ametoa somo kwa wasanii wa Afrika akidai kuwa mashabiki wazawa hawatoshi kumfikisha mbali msanii.
"Wasanii wapendwa msiruhusu kurasa za twitter na mashabiki wa mitandao ya kijamii wa Naija wawadanganye, hawawezi kujaza uwanja wowote kwa ajili yenu katika sehemu yoyote ya dunia"amesema Burnaboy.
Mbali na hayo ameeleza kuwa ni muhimu kwa wasanii kuhakikisha muziki wao unapenya zaidi kimataifa, kwani mapato ya streams za Ulaya na Marekani ni makubwa zaidi.
Hata hivyo, Burna Ametoa mfano kwamba streams milioni 1 Nigeria huleta dola 300hadi 400 ambazo ni sawa na sh 800K - sh 1 milioni za kibongo, wakati kiwango hicho Hicho Kwa Ulaya au Marekani kinaweza kuingiza hadi dola 3,000–4,000 ambazo ni sawa na sh 8 milioni hadi sh 10 milioni.
Hivyo Burna Boy amewataka wasanii waache kutegemea mashabiki wa nyumbani pekee, zaidi watafute tobo la kimataifa ili kutengeneza pesa ndefu zaidi.

Leave a Reply