Hali ya mwigizaji kutoka Ujerumani, Bruce Willis imeendelea kuwa mbaya, sasa ameripotiwa kupoteza kumbukumbu.
Willis, alibainika kuwa na maradhi ya Frontotemporal Dementia (FTD) mwaka 2023, aina ya ugonjwa wa akili unaoathiri sehemu za ubongo zinazohusika na lugha, tabia, mawasiliano pamoja na kumbukumbu.
Kwa mujibu wa familia yake, hali ya Bruce imeendelea kudorora, kiasi kwamba hawezi tena kuelewa umaarufu aliokuwa nao, wala kutambua mchango wake katika tasnia ya burudani. Mke wake, Emma Heming Willis, amesema mara nyingine humwangalia mumewe na kugundua kuwa hafahamu chochote kuhusu uigizaji.
“Tunamwambia kila siku jinsi alivyo mtu muhimu na jinsi alivyoacha alama kubwa kwenye maisha ya watu,” amesema Emma Heming
Licha ya hali hiyo, familia ya Bruce imetoa wito kwa umma kuelewa na kuongeza uelewa kuhusu maradhi ya FTD, ambayo bado hayajafahamika chanzo huku wakiahidi kutoa kitabu Septemba 2025 kitakachoelezea namna ya kuishi na mtu mwenye ugonjwa huo pamoja na kutambua tatizo hilo kwa haraka.
Bruce alianza kutambulika kupitia tamthilia ya Moonlighting (1985–1989) akicheza kama David Addison Jr ambapo filamu hiyo ilimfanikisha kunyakua tuzo ya Emmy na Golden Globe.
Pia ameonekana katika filamu mbalimbali ikiwemo Die Hard, Pulp Fiction (1994), 12 Monkeys (1995), The Fifth Element (1997), Armageddon (1998), The Sixth Sense (1999), na Glass (2019) huku filamu ya mwisho kuonekana ikiwa ni ‘Assassin’ iliyotoka Machi 2023.

Leave a Reply