Harmonize aishi kwa mashaka kisa wanawake

Harmonize aishi kwa mashaka kisa wanawake

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesema muda mrefu aliishi kwa hofu na mashaka juu ya watu aliokuwa akiingia nao kwenye mahusiano.

Amesema ulipoanza mwezi wa Ramadhani alimwambia Mungu nataka kufurahia muziki na maisha yake.

"Hata kama nikikutana na msichana mmeanza kupiga stori unaanza kumchunguza hajatumwa huyu. Nachukia haya maisha na mimeyachoka, sikutakiwa kuzungumza hivi lakini ilikuwa inanipa tabu, hata ninapotaka kuingia kwenye mahusiano na mtu sasa hivi I don’t care mtu akipanga amepanga yeye mimi nimemuachia Mungu,” amesema Harmonize na kuongeza.

“Ilikuwa inanipa wakati mgumu hata kuingia kwenye mahusiano. Nikiingia na mtu nilikuwa naonekana mimi nina wivu sana, kwa sababu lazima nijue nipo na mtu wa aina gani. Yaani nilikuwa naweza kuchukua simu yako, nikakuuliza unazungumza na nani ili tu kuangalia kama haujatumwa.”

Mbali na hayo, amegusia ishu ya deni alilokuwa akidaiwa na Benki ya CRDB.

“Ilikuwa changamoto kwa sababu siku hiyo habari inatoka, ndio naenda kutambulishwa ukweni. Kwahiyo unafika ukweni mkwe ana faili lako. Kwanza hakuna benki yoyote ambayo inanidai nadhani ilikuwa ni kutokuelewana kati ya sisi na CRDB ndio maana haujawahi kulisikia tena popote.

"Kwa akili zangu nilikopa na niliwashirikisha watu wangu wa karibu. Ni deni ambalo nilikopa wakati natoka Wasafi. Kwangu mimi nilichukulia kama changamoto,” amesema.

Utakumbuka Agosti 2024, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara ilimuamuru msanii wa muziki wa Bongofleva, Rajab Ibrahim, 'Harmonize' kuilipa Benki ya CRDB Sh113 milioni, zikiwa ni sehemu ya deni la mkopo anaodaiwa pamoja na fidia.

Mahakama hiyo ilitoa amri katika hukumu yake ya kesi ya madai iliyofunguliwa na benki hiyo baada ya msanii huyo kushindwa kurejesha deni la mkopo wa Sh300 milioni aliouchukua mwaka 2019.

Katika hukumu hiyo, Mahakama ilimuamuru Harmonize kuilipa benki hiyo Sh103.18 milioni ambazo ni sehemu ya deni la mkopo lililosalia na Sh10 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya jumla iliyoipata benki hiyo, kwa kitendo cha Harmonize kushindwa kumaliza kulipa deni hilo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags