Vijana wahimizwa kuonesha vipaji vyao

Vijana wahimizwa kuonesha vipaji vyao

Dar es Salaam. Jamii yahimizwa kuwashika mkono vijana wenye vipaji mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Mashindano ya vipaji kwa vyuo vikuu ya Unichampions, Elly Fadhili katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Fadhili amesema vijana hao kupitia vipaji vyao wanaweza kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto ya ajira kwa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

Pia amewahimiza vijana hao zinapojitokeza fursa za kuonyesha vipaji vyao kuzitumia ipasavyo.

Ametolea mfano mashindano ya wanavyuo ya Unichampions ambayo yanatarajiwa kuanza May 5, 2025 hadi Juni 27, 2025 na kuwahimiza kujitokeza kuonyesha uwezo wao.

"Mashindano hayo yatajumuisha michezo ya aina nne ambayo ni mpira wa miguu, itakayojumuisha timu 24 katika mkoa wa Dar es salaam,Basketball itakayojumuisha timu 16 za vyuo vikuu ,volleyball itakayojumuisha timu 16 pia,na Net ball ambayo pia itakuwa na timu 16"amesema.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa njia makundi kwa mpira wa miguu ambapo yatakua na timu tano kwa kila kundi na michezo hiyo itafanyika kikanda ambapo vyuo vipo.

"Tumegawanya makundi kutokana na timu hizi ambapo zipo wilaya ya Ubungo watatumia viwanja vya chuo cha Ustawi, ambazo zipo upande wa UDSM zitatumia uwanja wa UDSM na ambazo zipo upande wa Temeke vitatia uwanja wa DUCE Sambamba na timu zilizopo posta zitatumia uwanja wa Muhimbili."amesema.

Pia, Mwanakamati wa Tuzo za Kijamii, Ibrahim Shukrani amesema pamoja na michezo pia kutakuwa na tuzo za kijamii ambazo zitahusisha vipengele mbalimbali katika tuzo hizo ambavyo ni uongozi,ubunifu,uigizaji,uwasilishaj, upigaji picha,uandishi,ushawishi wa kijamii ujasiriamali,uwasilishaji wa hadhara,pamoja na uaandaji wa maudhui ambapo washindi watakua wawili katika Kila kipengele kwa kuzingatia jinsia zote mbili






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags