Jaivah Aanza Mwaka Na Story

Jaivah Aanza Mwaka Na Story

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Kautaka inayoendelea kufanya vizuri na kupenya kila kona Jaivah ameuanza mwaka kwa kutoa ngoma iitwayo ‘Story’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jaivah ameshare kionjo cha ngoma hiyo huku akiweka wazi kuwa wimbo huo ni mahususi kwa wote waliopoteza maisha kwenye harakati za kupambania maisha.

“Hii ni kwa ajili ya wanetu wote waliopoteza uhai wakiwa kwenye harakati za kutafuta maisha SOUTH AFRICA ama nje ya nchi. Sisi tuliozaliwa uswahilini tunajua tumepoteza ndugu,rafiki,jamaa/Masoja kibao kwenye harakati za kimaisha Bondeni,” ameandika Jaiva

Ujio wa msnaii huyo katika Bongo Fleva umeendelea kuitangaza Tanzania katika nchi mbalimbali hii ni baada ya nyota kutoka Nigeria Burna Boy na Mr Flavour kuonekana kukoshwa na wimbo wa ‘Kautaka’.

Toka aanze kufanya kazi za muziki Jaivah amewahi kutamba na ngoma kama Kautaka, Buruda, Soup na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags