Nyota kutoka klabu ya Al Nassr na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane ameweka wazi idadi ya watoto anaotamani kuwapata na mke wake Aisha Tamba.
Mane ameweka wazi suala hilo kupitia mahojiano yake na ‘Senepeoplus’ akieleza kuwa angependa kuwa na watoto wa tatu au wanne.
“Swali la kuchekesha sana, Ikiwa ni chaguo tu, ningesema 3 au 4. Isipokuwa kwamba ni Mungu anayeamua nami nitamshukuru bila kujali itakavyokuwa,” alisema Mane
Ikumbukwe kuwa Sadio Mane (32) na mke wake Aisha Tamba(19) walifunga ndoa Januari 2024 huko Keur Massar, Dakar huku wawili hao wakidaiwa kufahamiana kwa zaidi ya miaka 5 iliyopita.
Wakati wawili hao wanafunga ndoa Aisha, alikuwa na umri wa miaka 18 huku mwanasoka huyo akimzidi mke wake miaka 13.
Leave a Reply