Jiongeze: Wake Wa Jenzii Fanya Haya Usilie Tena

Jiongeze: Wake Wa Jenzii Fanya Haya Usilie Tena

Kizazi kipya wengi hawana elimu. Inayohusu jinsi ya kuishi kwenye ndoa. Ndo maana ‘deile’ ndoa zinavunjika kama biskuti iliyolowana. Sasa pata somo hapa lisha jiongeze kivyako. Na ndoa ikakaa sana usinipe posho wala asante.

Mheshimu mumeo. Hata akichepuka usifungue mdomo. Ongeza upendo ataona aibu mwenyewe ataacha. Na ule ‘umjinimjini’ achana nao. Maneno ya salon, mashoga na majirani achana nayo. Usiombe ushauri kwa mashosti juu ya mumeo.

Epuka marafiki ambao hawana ndoa.
Ukiwaeleza ya ndani watakupotosha ili muachane. Ili uwe kama wao na pengine hata kukuibia mume kabisa. Kumbuka nao hutamani wawe kama wewe. Usioneshe hasira ukikosewa na uwe wa kwanza kuomba radhi.

Badili sauti umuonapo mumeo. Ongea sauti ya unyenyekevu. Usipende kuwa juu yake. Kama upo’ ‘homu’ na huna kazi, usiache kazi afanye dada wa kazi. Kama, kupika na kufua nguo za ndani za baba, kufanya usafi ‘rumu’ kwa baba iwe marufuku.

Usipende kumuuliza, kama ametoka wapi saa hizi? Kwanini umechelewa? Mbona kwenye shati kuna rangi ya ‘lipsticki’? Usiguse simu yake bila idhini yake. Hata aongeapo na simu usimuulize umeongea na nani mpe uhuru. Ni ngumu ila ndo dawa.

Jaribu kuwa mtu wa stori nzuri nzuri. Usimsimulie mume stori za watu sijui nani kagombana na nani. Yaani ule umbea umbea wenu wa kijinga acha. Jaribu kuwa karibu na familia yake, kama ‘kuwasapraizi’ wakwe zawadi ndogo ndogo. Muhimu sana hii.

Kama kuna mashemeji wanasoma wapige tafu hata kama ni kidogo. Ule ukarimu watakaoweka kwako hakika mumeo atapenda. Haswa pale mama akimpigia simu mwanaye kumwambia mwanangu umepata mke.

Au madogo kumpigia braza wakiwa na shida. Shemeji yao ukiimaliza hiyo shida, hata mumeo apatapo habari kama hizo huongeza upendo sana. Fuata hayo ninayokuambia. Utaishi na mumeo kwa raha mustarehe mpaka wabaya wako roho ziwapasuke.

Ndoa hiyo ikivunjika njoo unihukumu. Nawapenda sana wanawake Mungu awasaidie katika ndoa zenu. Na hapa nalazimika kuwa ‘ticha’ kwa sababu ndani ya wiki moja. Ndoa tano za rafiki zangu zimevunjika. Sababu zao ni za kijinga jinga tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags