Diamond Aweka Historia Marekani

Diamond Aweka Historia Marekani

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameandika historia nyingine kwenye muziki huo, ambapo usiku wa kuamkia leo Juni 21, 2025, amefanikiwa kutumbuiza katika tamasha kubwa la ‘Hot 97 Summer Jam’ lililofanyika jijini Newark, New Jersey nchini Marekani.

Diamond anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza katika tamasha hili kubwa la ambalo kwa miaka mingi limekuwa likiwapokea mastaa wakubwa kama Jay-Z, Nicki Minaj, Drake, Cardi B, Nas, Lil Wayne na wengineo.

‘Hot97 Summer Jam’ ni moja ya matamasha yenye heshima kubwa katika muziki wa kimataifa, hasa kwenye muziki wa Hip Hop, R&B, ambapo nasasa imevuka mipaka kwa na kuukaribisha muziki wa Bongo Fleva kushiriki katika jukwaa hilo.

Aidha wakati alipokuwa kwenye mahojiano ya chombo cha habari kikubwa Marekani ‘TMZ’ msanii huyo aliweka wazi kuwa ametumia zaidi ya dola 250K ikiwa ni sawa na Sh663 milioni kwa ajili ya kufanikisha show hiyo kwenda kama alivyo tarajia.

Katika tamasha hilo Diamond aliungana na wasanii wengine kama Ayra Starr, Gunna, Asake, JaRule, Glorillapimp, A-Boogie na wengineo wengi.

Hata hivyo kabla ya kuonesha balaa lake katika jukwaa hilo msanii huyo mapema jana alikabidhiwa Tuzo ya ‘Diamond Play Button’ kutoka Youtube ambayo inatolewa kwa chaneli zilizofikisha au kupita subscribers milioni 10.

Mafanikio haya yanamuweka kwenye nafasi ya nzuri msanii huyo sit u ndani ya Bongo au Afrika Mashariki lakini pia Kimataifa ambapo wasanii watatu tu wa Kiafrika wameweza kufikia kiwango hicho kwenye Youtube ambao ni Mohamed Ramadan, Saad Lamjarred Na Soolking.

Mbali na tukio hilo Juni 14, 2025 aliweka historia mpya jijini London baada ya kuujaza ukumbi wa Royal Albert kwa kuingiza mashabiki zaidi ya 5000 na kupisha show ya kukata na shoka.

Kupitia mafanikio ya shoo hiyo, pia Diamond ametunukiwa cheti na uongozi wa Royal Albert nchini humo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kumbi kubwa duniani kufanya hivyo kama ishara ya kumpongeza msanii kwa mafanikio ya kuuza tiketi zote na kujaza ukumbi kwenye show yake.

Katika shoo hiyo ambayo Diamond aliambatana na familia yake akiwemo Mama Dangote, msanii huyo alifanya sapraizi ya kuwapandisha wasanii kama Tiwa Savage, Mr Flavour, Patoranking, Jux, na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags