Mwigizaji Damson Kuwa Mrithi Wa Chadwick

Mwigizaji Damson Kuwa Mrithi Wa Chadwick

Mwigizaji maarufu kutoka Uingereza mwenye asili ya Nigeria, Damson Idris, ameendelea kupenya katika tasnia ya filamu ya Hollywood, hii ni baada ya kuthibitisha kuwa mmoja wa wahusika watakao onekana kwenye filamu ya Black Panther 3.

Damson, ambaye amejulikana zaidi kupitia uhusika wake kama Franklin Saint kwenye mfululizo wa Snowfall, anatajwa kama mmoja wa nyota wapya watakaoleta mvuto mkubwa katika muendelezo wa filamu hiyo ya Marvel Studios.

“Kuwa sehemu ya urithi huu mkubwa ni heshima kubwa kwangu binafsi na kwa jamii yangu. Black Panther si filamu tu, ni ishara ya nguvu na umoja wa Waafrika duniani.

Ninajua mashabiki wana matarajio makubwa, na naahidi nitajitahidi kutoa kila kitu ili kutoa heshima kwa waliyotangulia na kuleta kitu kipya kitakachogusa mioyo ya watu,” amesema Damson

Aidha ujio wake kwenye Black Panther 3 umeibua mijadala mikubwa mitandaoni, wengi wakitarajia ataiendeleza heshima iliyoachwa na marehemu Chadwick Boseman.

Chadwick Boseman alifariki dunia Agosti 28, 2020 akiwa na umri wa miaka 43 alifariki kutokana na saratani ya utumbo mpana (colon cancer), ambayo alikuwa akipambana nayo kwa siri kwa miaka kadhaa.

Enzi za uhai wake Boseman alitambulika kupitia uhusiaka wake kama King T’Challa katika filamu ya Black Panther, huku akiitendea haki filamu hiyo pamoja na kuitambulisha Afrika Kimataifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags