Baada ya zaidi ya wiki sita za ushahidi mzito dhidi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean “Diddy” Combs, sasa kesi hiyo imefungwa huku ukisubiliwa uamuzi wa mahakama.
Hatua hiyo ya kufungwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka ulifanyika Jumanne 24, 2025 baada ya wakili wa Diddy, Teny Geragos, kumaliza kumhoji shahidi wa mwisho wa serikali, Joseph Cerciello, afisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Usalama wa Ndani (Homeland Security Investigations).
Hata hivyo kufungwa kwa kesi hiyo pia kunakuja baada ya upande wa Diddy kuweka wazi kutosimamisha shahidi wowote wa utetezi. Aidha katika siku hiyo hiyo waendesha mashtaka waliendelea kusisitiza kuwa vitendo vya kingono vilivyokuwa vikifanywa ya Combs ni ushahidi tosha wa kumuhukumu msanii huyo.
Combs, mwenye umri wa miaka 55, ameendelea kusisitiza kutokuwa na hatia tangu kukamatwa kwake Septemba mwaka jana, amekuwa rumande katika gereza la shirikisho huko Brooklyn, bila kupewa dhamana huku majaji kadhaa wamekataa maombi ya dhamana kwa madai kuwa Diddy ni tishio kwa usalama wa jamii.
Kesi hiyo sasa imeingia katika hatua ya mwisho huku mashabiki, wanahabari, wanasheria na mashabiki wa rapa huyo wakiusubiri uamuzi wa mahakama.

Leave a Reply