Mwigizaji wa Jua Kali Kitundu afariki dunia

Mwigizaji wa Jua Kali Kitundu afariki dunia

Mwigizaji wa Jua Kali Raidanus Vitalis ‘Kitundu’ amefariki dunia Juni 24,2025.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na mzalishaji na mwongozaji wa tamthilia ya Jua Kali Leah Mwendamseka 'Lamata' kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Umeniweza Kitundu.Lamata village tunasikitika kumpoteza msanii wetu wa Jua Kali leo hii jioni. Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi,” ameandika Lamata kupitia ukurasa wake wa Instagram

Enzi za uhai wake Kitundu aliigiza kwenye tamthilia hiyo kama kijana mwenye kipaji cha kucheza muziki anayetokea kwenye familia ya kimasikini. Kisha baadaye anapata nafasi ya kutoboa kimaisha lakini anashindwa kuitumia vizuri na kujikuta akirudi kwenye maisha ya kimasikini.

Hadi sasa bado chanzo cha kifo chake hakijafahamika. Mwananchi inaendelea kufanya juhudi za kuwatafuta watu wa karibu wa marehemu. Apumzike kwa amani Kitundu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags