Msanii wa hip hop kutoka Marekani, Kid Cudi, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoa ushahidi dhidi ya mwanamuziki na mfanyabiashara “Diddy” Combs, akieleza kuwa hakuwa na nia ya kutoa ushahidi bali alilazimishwa.
Cudi ambaye jina lake halisi ni Scott Mescudi, wakati alipokuwa kwenye mahojiano katika kipindi cha ‘Call Her Daddy’ amesema kuwa mara ya kwanza alipoombwa kwenda kutoa ushahidi alikataa hadi pale alipolazimishwa kwa wito wa mahakama (subpoena).
“Nilikuwepo pale kwa sababu nililazimika. Mara ya kwanza waliniomba, nikasema hapana. Waliniomba tena, nikasema hapana. Kisha nikapewa wito wa mahakama (subpoena) nikasema, sawa, Sikutaka kabisa kufanya hivyo nilichukia kila dakika,”amesmea Cudi
Aidha nyota huyo wa ‘Pursuit of Happiness’ aliendelea kwa kueleza kuwa aliamua kutoa ushahidi kwa lengo la kumsaidia rafiki yake na mpanzi wake wa zamani Casandra “Cassie” Ventura. “Niliamua kutoa ushahidi kama njia ya kumsaidia Cassie, rafiki yangu, kumlinda na kumsaidia kufanikisha mambo yake. Nilitaka tu kumwona akistawi na kuwa na furaha,”alisema
Utakumbuka Kid Cudi alitoa ushahidi mahakamani dhidi ya Sean “Diddy” Combs mwezi Mei 2025, ambapo aliweka wazi kuwa mwaka 2011 Diddy alivamia nyumba yake na kisha kumfunga mbwa wake bafuni, lakini pia mwaka 2012 alidai kuwa gari yake lilipuliwa na bomu aina ya Molotov cocktail. Waendesha mashtaka walidai tukio hilo lilihusiana na Combs, ingawa Cudi hakumtaja moja kwa moja kuhusiana na mlipuko wa gari.
Ikumbukwe Diddy alipatikana na hatia mapema Julai kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya kushiriki katika vitendo vya ukahaba. Mahakama ilieleza kuwa aliwasafirirsha wapenzi wake wa zamani na watoa huduma wa kiumbe katika maeneo mbalimbali ya Marekani kwa ajili ya matukio ya kingono.
Aidha alifutiwa mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kula njama ya kufanya uhalifu (racketeering conspiracy), kulazimisha watu kwa ajili ya ngono mashtaka ambayo kama angepatikana na hatia kungekuwa na uwezekano wa kifungo cha maisha jela.
Mara baada ya kuondolewa mashitaka hayo Julai 2, 2025 wakili wake aliomba atolewe kwa dhamana, lakini Jaji Arun Subramanian alikataa, akisema ushahidi wa Diddy bado haupo wazi kwamba si hatari kwa mtu yeyote na jamii. Ambapo sasa wakili huyo amekuja tena na ofa nono ya dhamana ya dola milioni 50 pamoja na bondi ya nyumba ya Diddy iliyopo Miami, lakini ombi hilo lilikataliwa.
Kwa sasa, Diddy ameingia katika orodha ya watu maarufu waliowahi kufungwa katika gereza la MDC Brooklyn. Gereza pekee la shirikisho jijini New York, ambapo mastaa wengine waliowahi kuwepo ni pamoja na mwimbaji R Kelly, Ghislaine Maxwell na mfanyabiashara wa sarafu ya kidijitali Sam Bankman-Fried nk. Diddy anatarajiwa kuhukumiwa Oktoba 3,2025.

Leave a Reply