Mmiliki mpya wa maiki hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake hadharani amesema ana matumaini ya kuuza maiki hiyo kwa dola milioni moja za Marekani (zaidi ya Shilingi bilioni 2 za Kitanzania), huku akidai kuwa tayari ameshapokea ofa ya dola 40,000 (takriban Shilingi milioni 104), hivyo anaamini hatakaa nayo kwa muda mrefu.

Hapo awali maiki hiyo iliuzwa kwa dola 2,550 (takribani Shilingi milioni 6.6) baada ya mmiliki wa kwanza, Scott Fisher, kushindwa kuiuza kwa bei ya juu aliyoitangaza ya dola 100,000 kutokana na watu waliokuwa wakipandisha bei kwa utani mitandaoni.
Mmiliki wa sasa amesema alimfuata wakili wa mwanamke ambaye amemfungulia kesi Card akimpa kipaumbele ili aweze kuinunua kabla haijatangazwa lakini amesema kuwa mwanadada huyo aliyefahamika kwa jina la Jane Doe hakuonesha nia yoyote. Hivyo basi amepanga kuiuza maiki hiyo kupitia mtandao wa eBay.
Katika tangazo lake, muuzaji huyo amesema sehemu ya fedha zitakazopatikana katika mauzo hayo atazitoa kama msaada kwa shirika la kutetea haki za watu weusi nchini Marekani (NAACP).
Inadaiwa kuwa maiki hiyo imerudi tena sokoni baada ya Cardi kuzungumziwa sana mitandaoni kufuatia na ushiriki wake kwenye onesho la WWE SummerSlam wiki iliyopita pamoja na kutangaza albamu yake mpya. Ikumbukwe wiki chahce zilizopita Jane Doe alirudisha kesi hiyo tena mahakamani akidai fidia kutokana na msongo wa mawazo na maumivu ya kihisia aliyoyapata katika tukio hilo.
Hata hivyo, Cardi B na wakili wake Drew Findling wamepinga vikali madai hayo, wakidai kuwa kesi hiyo ni hila tu ya kutaka kupata fedha kirahisi. Pamoja na hayo, mchakato wa kesi bado unaendelea mahakamani hadi sasa.
Leave a Reply